Cart 0
 
 
 
 
 
Upo mahali gani katika safari yako ya kirohona Yesu?
 
 
sunset-banner_1200x800.jpg

 

Nina dadisi kujifunza zaidi

 

Mimi na wewe tunafanana.

Grape Vector 5.png

Mimi na wewe, na kila binadamu awaye yote katika sayari hii ya dunia anayo mahitaji muhimu matatu: hitaji la kupendwa , hitaji la kuhitajika , na hitaji la kukubalika.

Vipi kama nitakueleza ninajua ni kwa namna gani unaweza kupata mahitaji yote hayo matatu na kwa kutosheleza?

Vipi kama nitakueleza kwamba siuzi kitu hata kimoja kati ya hivo?

Vipi kama nitakueleza mahitaji yote haya matatu hayapatikani kwa ujira,kwasababu yenyewe ni zawadi?

Unaona, kulikuwa na wakati katika maisha yangu ambapo sikuwa na amani, kusudi na tumaini sasa ninayo furaha. Nilikuwa nikiutazama ulimwengu nikitumainia mengi katika maisha zaidi ya hili.

Lakini mtu Fulani akachukua mda wake kuniambia habari za Mungu ambaye ananipenda hata upeo na analo kusudi na tumainikwaajili ya maisha yangu. Huyu si Mungu aliyekuwa mbali na aliye mbali,Lakini ni Mungu anayenitaka mimi niishi pamoja naye daima mbinguni pale ntakapokufa.

Lakini ninalo tatizo. Mbinguni ni kukamilifu na mimi sio! Kwahivo siwezi kuingia mbinguni. Lakini huyu Mungu amenifanyia njia kupitia mwanawe Yesu Kristo kuja duniani na kufa kwaajili ya dhambi zangu. Na kasha baada ya siku tatu alifufuka tena, akiithibitisha kwamba nikweli yeye alikuwa chambo.

Kwahivo nimemwalika Yesu awe dereva wa maisha yangu. Nimemwomba anisamehe pale nipokosea, na nimemwomba nguvu ili niishi katika yeye, na sio kwaajili yangu.

Na unajua kitu gani kilitokea? Nimepokea tumaini jipya, amani na kusudi.Ilikuwa nizaidi ya kawaida .Na bado haijakoma.


Sasa vipi kuhusu wewe? 

Question Vector 1.png

Upo tayari kwaajili ya mwanzo mpya katika maisha? Biblia inasema kwamba tunapomkiri Yesu kuwa Bwana wa maisha yetu, tumekuwa kiumbe kipya… ya kale yote yamepita na kila kitu kimekuwa kipya!

Hapa ni swali?

“Kitu gani kitakuzuia kutosalimisha maisha yako kwa Yesu leo?”

Hofu? Huna uhakika? Unao msukumo? Oh ni rahisi tu, pengine unakwepa kufikiri masuala ya umilele? Pengine unadhani Mungu anamasuala mengine mengi ya muhimu kufanya?

Hii ni habari njema. Mungu anakupenda! Na ikiwa tutatubu dhambi zetu kwa Yesu, Atazisamehe zote…wakati… haijalishi dhambi ni kubwa au ndogo kiasi gani. Kwanini unabahatisha na kusubiri?

Sikiliza KATs tuambie unaendaje mbinguni:

Kubali Nimetenda uovu. Mimi ni mwenye dhambi. Na Mungu hawezi kuruhusu hata dhambi moja ndogo iingie mbinguni, au haiwezi kuwa mbinguni.

Amini moyoni mwangu kwamba Yesu halisi alikuja kufa kwaajili ya dhambi zangu, na akafufuka, akithibitisha kweli alifanyika chambo.

Tubu dhambi zangu na omba msamaha wake. Hitaji kubadilika katika dhambi kwa msaada wa Mungu. Kiri Yesu ni bwana na mwokozi wangu… Bosi wangu.

Huwezi kusafisha maisha yako kabla hujaja kwa Mungu.Ni lazima uje jinsi ulivo. Yeye hana hisia na usafi wetu au matendo mema, kwasababu yeye hana dhambi,anatualika tusamehewe na tuwe huru!

Unafikiri nini,kitu gani kitakuzuia usimwombe Yesu kuwa mfalme wa maisha yak oleo? Hakuna?

Kisha, Utaomba ombi hili kutoka moyoni sasa?

Endelea na omba kwa sauti sasa kama unamaanisha kutoka moyoni:

“Yesu mpendwa,
Ninakiri nimetenda kinyume, na kwahilo mimi ni mwenye dhambi. Ninatubu dhambi zangu. Ninaamini ulikufa kwaajili yangu na kufufuka tena. Natubu dhambi zangu kwako. Nisamehe na unipe mwanzo mpya. Nakuomba uwe bwana na bosi wa moyo wangu. Nisaidie sasa niishi kwaajili yako, Asante kwa upendo wako mkuu na msamaha. Nimeomba haya katika jina la Yesu amina!”

 

Hongera! 

Kama umemaanisha ombi hilo kutoka moyoni mwako,basi Mungu amekusikia sasa.Amekusamehe katika kila ovu na dhambi ulizotenda. Haijalishi dhambi yako ilikuwa kubwa au ndogo, imesamehewa. Na sasa umekuwa na mwanzo mpya …tiketi mpya!

Na hapa nikwa jinsi gani unaweza tunza upendo wa Mungu kimwili na imara:

Question Vector 2.png

Soma Biblia yako na omba kilasiku. Ningelipenda kukutia moyo kuanza kusoma kitabu cha mtakatifu Yohana. Kitakuelezea yote kumhusu Yesu na jinsi alivo mwema kwako. Na maombi ni kuzungumza na Mungu kirahisi zaidi. Mshukuru kwa mambo mema katika maisha yako, na muombe hekima upitiapo magumu katika maisha.

Tafuta kanisa la kusali ambalo linaamini Biblia ni kweli, na kuhubiri kuhusu kumjua Yesu kama ambavyo sasa unatenda. Kama unahitaji msaada, nitumie ujumbe nami ntakusaidia.

Batizwa kwa maji. Utakusaidia kuweka chapa moyoni mwako na kuwa imara na kjitoa kwako kutaimarka.Kanisa lako litakusaidia katika hili.

Jazwa na Roho Mtakatifu. Muombe Mungu akujaze Roho Mtakatifu kila siku,na kuachilia kipawa chake kwako.Sura 5 za kwanza katika matendo zitakusaidia.

Mwambie mtu yeyote mara nyingi uezavyo juu ya maombi yako leo, na jinsi Mungu alivokusamehe.

Sasa, jambo moja zaidi.Utanitumia barua pepe leo kupitia frostygrapes@oasiswm.org, na ukinieleza juu ya uamuzi wako wa kumfanya Yesu kuwa mfalme wa moyo wako. Inawezekana hujawahi kufanya hili nah ii ndo mara yako ya kwanza au labda unashangaa hukuwa Roho Mtakatifu lakini sasa umerudi nyumbani. Kwa jambo lolote ningelipenda kusikia kutoka kwako.

Hizi ni baadhi tu ya tovuti ambazo zitakusaidia kukua katika imani yako mpya nay a kuvutia: www.ushuhudawadakikamoja.org, and www.oasisworldministries.org.