Sina Nia
Kitu gani kitakuzuia usisalimishe maisha yako katika mamlaka na upendo wa Yesu Kristo, Mungu pekee aliyekufa kwaajili yako?
Hapa kuna sababu nne ambazo watu wengine hutoa:
“Sipo tayari.”
Vizuri, upo tayari kufa usiku bila ya kusamehewa? Kama sivo, basi upo tayari kumkubali Yesu sasa. Kama tu ilivo yupo Mungu akupendaye upeo, basi yupo pia shetani akuchukiaye balaa. Atakupa aina zote za sababu na ili usitoe maisha yako kwa Yesu. Na hii ndiyo sababu Biblia inamwita ‘baba wa uongo.’
Au labda hauko tayari kuzikatia tama dhambi zako katika maisha. Hilo sio jambo jipya. Wote tunapaswa kuishi kwa Yesu katika mda na siku moja. Kama dhambi yako pendwa itakutenga na upendo wa Mungu na kuwa nje ya mbingu, Je itakuwa na faida? Na kila dhambi utakayo ikatia shauri nafasi yake itachukuliwa na furaha kuu na amani ndani ya moyo wako. Naahidi.
Endelea. Mfikie Mungu kwa imani, na achana na udhuru miongoni mwako. Atakusaidia kila siku.
“Mungu anayo mambo mengi zaidi ya muhimu kuliko maombi yangu...”
Tafakari kuhusu hilo. Unadhani Mungu anayemiliki ulimwengu mzima anaweza kujibu maombi 20 tu kwa siku? Unadhani utapaswa kusubiri katika foleni ya mstari? Au kusafisha maisha yako kwanza kabla Mungu hajakusikia?
Biblia inasema kwamba yeye hataki hata mtu mmoja (WEWE) akose mbinguni. Kama ulikuwa ni mtenda dhambi pekee ulimwenguni, bado angelikuja tu duniani afe na afufuke tena ili upate kusamehewa!
Yeye ni mvumilivu anakusubiri wewe umfuate. Kila asubuhi jua lichomozapo, anazungumza na wewe akikuonyesha mema yake. Usisubiri siku nyingine. Hujui siku yako ya mwisho hapa duniani itakukuta wapi. Utaweza kuwa na hakikika unakwenda mbinguni kupita kumuita yeye tu.
Ikiwa hilo ni hitaji lako, tembelea "NINA-DADISI-KUJIFUNZA-ZAIDI" kifungu.
“Nimetenda dhambi sana.”
Kiasi gani ni zaidi? Mungu anatuanisha kama “watenda dhambi waliokithiri” au “watenda dhambi wazur”?
Kulingana na Biblia, sote tumetenda dhambi,hivo hakuna hata mmoja atakaenda mbinguni, kama sivo basi mbingu isingekuwa thabiti tena. Haijalishi dhambi zetu ni kubwa au ndogo, sote tumekosa sifa. Sote tumetenda dhambi.
Lakini upendo wa Mungu unafunika dhambi zote. Hata kama Yesu alikufa msalabani, wauwaji wawili walisulubishwa naye pia. Mmoja akamcheka Yesu, lakini mwingine alimuomba Yesu amsamehe. Na Yesu akasema umesamehewa.
“Mimi ni mtu mwema kiasi… kwa hakika si mbaya kama watu wengi walivo.”
Matendo yako mema yatakupeleka mbinguni? Unayohakika kweli umetenda mema vyakutosha? Kuna maeneo mawili ambayo ni matatizo katika hili.
Moja ni swali,ni matendo mema mangapi ninapaswa kufanya ili nipate kuingia mbinguni? Vipi kama ninalo tendo jema moja fupi?
Ugumu mwingine ni, ‘Kama naweza kuingia mbinguni kwa matendo mema, kwanini Yesu alikuja duniani na kufa?’
Biblia inatufundisha kwamba huwezi kipata mbingu kwa kazi au ujira… ni zawadi! Lakini napaswa kuifikia na kuipokea kwa imani.
Matendo mema ni muhimu sana, lakini yenyewe tu hayawezi kufuta dhambi zetu. Yesu pekee kwa matendo yake msalabani anaweza kutusamehe sisi.
Hivo, udhuru unatosha? Ni muda wa kumuita Mungu na kumuomba awe msaada katika maisha yako. Muombe akusamehe an afanyike kuwa bwana wako, mwokozi na bosi wa maisha yako. Utakuwa ni uamuzi bora kuwahi kufanya.
Tembelea "NINA-DADISI-KUJIFUNZA-ZAIDI" kifungu, na unaweza kusali sala amayo itabadili moyo wako daima!